RAIS DKT. SAMIA AZUNGUMZA NA MAWAZIRI WA MICHEZO KUTOKA KANDA YA NNE YA AFRIKA KUPITIA VIDEO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu kwa njia ya video fupi ambapo amewakaribisha Mawaziri wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kwenye Mkutano wa kwanza wa Kanda hiyo kufanyika hapa nchini.
"Huu ni mkutano wa kwanza wa kihistoria wa Kanda ya IV kufanyika katika ardhi ya Tanzania. Tunawakaribisha Wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV hapa nchini kwetu ambayo ni Nchi ya amani na ukarimu ikiwa na vivutio vingi vya Utalii Bora Duniani" Amesema Rais Dkt. Samia.
Amesema miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni kuchagua nchi ambayo itakuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wajumbe wa wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV kuwa Tanzania ipo tayari kuwa Makao Makuu ya Baraza hilo.
Akitoa mfano, amesema Tanzania ni nyumbani kwa Taasisi za kimataifa, hivyo Ina Kila sababu ya kuwa mwenyeji wa Baraza hilo ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Sekretariti hiyo.
"Naleta ombi kwenu ninyi Mawaziri wa Michezo mliopo hapa muipe Tanzania jukumu hili kwa mwitikio chanya kwa ombi letu" amesema Rais Dkt. Samia.
Rais Dkt. Samia.ameongeza kuwa wajumbe wa mkutank huo kutenga muda wa kutembelea vivutio mbalimbali ambavyo Tanzania imebarikiwa kuwa navyo ili wajue Tanzania inaweza kutoa nini kwa Afrika na Dunia.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.