RAIS SAMIA ALIPIA GHARAMA WASHIRIKI KUTOKA ARUSHA WANAOIWAKILISHA TANZANIA MASHINDANO YA PIKIPIKI AFRIKA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa tiketi za ndege kwenda na Kurudi nchini Morocco kwa washindi watatu wa mashindano ya Pikipiki ya Samia Motocross Championship kwaajili ya kushiriki mashindano ya FIM Africa Motocross of African Nations yanayofanyika Oktoba 25- 27, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo mapema leo Oktoba 22, 2024 Ofisini kwake Jijini Arusha wakati akiwaaga washiriki wa mashindano hayo, wanaoondoka leo Jioni kupitia shirika la ndege la Qatar Airways mapema leo Jioni kupitia uwanja wa ndege wa Arusha.
Wanaoondoka Jioni ya leo ni Wachezaji Kelvin Akyoo, Simon Mangombo pamoja na Colins Simonson ambapo wameambatana na Kiongozi wao Mmoja pamoja na mwanahabari Doto Kadoshi, wakiahidiwa Kukutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan watakaporejea ikiwa watafanya vizuri kwenye mashindano hayo makubwa barani Afrika yanayotarajiwa kufanyika Mjini Marrakech nchini Morocco.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.