Na Elinipa Lupemne
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya vikundi vya vijana walioshiriki kwenye Maonesho ya wiki ya Vijana Kitaifa na Kumbukizi ya Miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa kutoka kwa Kaimu Afisha Vijana mkoa wa Arusha, Hanifa Ramadhani mara alipotembelea Banda la Vikundi vya vijana mkoa wa Arusha.
Akimkaribisha Mheshimiwa Rais Hanifa amesema kuwa katika banda la mkoa wa Arusha jumla ya vikundi tisa vya vijana vilivyonufaika na mikopo ya bila riba kupitia asilimia 4 ya Mapato ya ndani ya halmashauri.
Maonesho ya wiki ya Vijana Kitaifa yamehitimishwa leo ikiwa ni kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mw. Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 yenye Kauli mbiu ya Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.
#Arushafursalukuki
#kaziinaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.