Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia amekabidhi fedha taslimu shilingi Milioni 10 kwa Mkurugenzi wa halmshauri ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya, fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kikatiti.
Fedha hizo aliziaidi Mhe. Samia Suluhu Hassan Octoba 16,2021 aliposimama njiani kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Kikatiti alipokuwa akiwasili Mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhe. Rais alizitoa fedha hizo kama mchango wa kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kikatiti ambayo ujenzi wake umeanza kutokana na nguvu za wananchi.
Aidha, Katibu Tawala amewataka viongozi wa Halmashauri ya Meru na Kijiji hicho kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyoelekezwa na Mhe.Samia na si vinginevyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.