Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni maafisa wanafunzi 118 kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli kwa cheo cha Luteni usu na maafisa wanafunzi 61 wa shahada ya kwanza ya mafunzo ya kisayansi ya kijeshi kutoka chuo cha uhasibu Arusha (IAA).
Sherehe hizo za mahafari ya pili ya mafunzo ya kijeshi zimefanyika katika viwanja vya chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli na kihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali.
Maafisa waliotunukiwa Kamisheni kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli maafisa wanafunzi 61 wamepata shahada ya sayansi ya kijeshi na 56 wamepata shahada ya jeshi la anga, ambapo wanaume walikuwa 99 na wanawake 19.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.