Katika kusherehekea miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ametumia muda huo kuzungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uzinduzi uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 09 Desemba, 2023.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.