• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RAIS SAMIA AZITAKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUJITEGEMEA KATIKA KUPAMBANA NA MAJANGA YANAYOTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Posted on: November 23rd, 2023


Na Prisca Libaga.

RAIS Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutotegemea wahisani kutoka ughaibuni kama misaada ya kupambana na majanga yatokanayo  na mabadiliko ya hewa

Alisema bara la Afrika ni mama wa mazingira hivyo nchi za EAC zisikubali tena kuharibu mazingira kwa kutegemea misaada ya kifedha kutoka nchi.

RAIS alisema hayo jana kwenye Mkutano wa ngazi ya juu wa 23  wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha wakati akiwahutubia viongozi mbalimbali wakiwemo marais watatu na wawakilishi wa marais 3 wa EAC

"Tusiwategemee wengine kuja kutupa fedha za majanga ya mabadiliko ya hali ya hewa.Nashauri huu uwe ujumbe wetu kwa nchi za EAC kwenye mkutano ujao wa dunia wa COP28 kuhusu mazingira" alisema

Alisema bara la Afrika bado lina mazingira mazuri  sana na kuna fursa hivyo mataifa ya nje wanapenda kuja kutumia rasilimali  hivyo nchi za EAC zinatakiwa kuanza kutumia mapato yake kwenye majanga ya tabianchi

"Wenzetu huko wameishaharibu hawana mazingira  tena. Tunatakiwa kulinda mazingira yetu, hivyo tukatae masharti. Haiwezekani sisi tunalinda halafu makampuni ya nje yanakuja kuvuna" alisema

Rais pia alizitaja  juhudi mbalimbali zinazofanywa na  serikali katika kukabiliana na majanga ya mabadiliko ya tabia nchi

Baadhi ya  juhudi hizo ni pamoja na serikali kuondoa kodi kwenye pembejeo za kilimo kwa ajili ya kukuza kilimo na usalama wa chakula, kuondoa ushuru na vivutio vyote vya kodi kwenye bidhaa zinazotumika kuzalisha nishati mbadala kwa ajili ya kulinda mazingira.

"Sasa hivi tunahamasisha sekta binafsi kuchangamkia fursa zinazotokana na majanga ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuanzisha vituo vya utafiti nchi nzima. Hapa tunataka sekta binafsi washiriki kwa kuongeza thamani bidhaa za mazao ya kilimo" alisema

Kwa Upande wake  Mwenyekiti anayemaliza muda wa EAC RAIS wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye alisema dunia iko kwenye matatizo makubwa ya ukame na mafuriko hivyo nchi za EAC lazima zinatakiwa kwa pamoja kuja upya na sera mpya zitakazozinusuru kutoka kwenye janga la mabadiliko ya tabia nchi.

"Tunahitaji kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za dni na wadau wengine wa maendeleo" alisema

Alisema mahitaji makubwa kwa nchi za EAC ni kuwa na teknolojia, uafiti wa kina na uwekezaji katika masuala ya mazingira

"Ili kuwa na usalama wa chakula lazima tuwekeze kwenye utafiti na teknolojia na tunahitaji sera ya kanda kuhusu mabadiliko ya tabia nchi" alisema

Mkutano wa Wakuu wa Nchi unahirishwa jana kwa Rais wa Ndayishimiye kukabidhi kijiti kwa Rais Salva Kiir wa Jamhuri ya Sudan   Kusini. Katika mkutano huu Marais Paul Kagame (Rwanda),  Felix Tshekedi ((DR Congo) wametuma wawakilishi

Mwisho





Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.