Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma Nchini.
Hayo yamesemwa leo tarehe 18/08/2023 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John V.K Mongella alipokuwa akizungumza na Vyombo vya Habari katika ukumbi wa mbayuwayu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Sambamba na hilo,tarehe 21/08/2023,Rais wa Dkt, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira Usa-River Wilayani Arumeru.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania lilianzishwa rasmi tarehe 19/06/1963 baada ya muungano wa Makanisa saba ya Kilutheri yaliyokuwepo Nchini Tanzania kabla ya mwaka huo na mpaka kufika mwaka huu 2023 Kanisa hilo linatimiza miaka 60 ya huduma yake likiwa na Dayosisi 27.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.