Na Elinipa Lupembe
Eneo la lililozunguka ziwa Eyas maarufu kama Lake Eyas kijiji Langhangareni kata ya Mango'ola wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha, liko umbali wa takribani Km 67 kutoka makao makuu ya wilaya, ni takribani mwendo wa zaidi ya saa moja kwa gari.
Katika hali isiyo ya kawaida kwa wananchi wa kijiji cha Langhangareni, Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kujenga shule mpya ya sekondari, kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari nchini ( SEQUI)
Wananchi hao wamemshukuru Rais mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa kijiji chao kuwa na shule, kwa kuwa watoto wao sasa watasoma sekondari kama ilivyo kwa watoto wengine wa kitanzania.
Wamesema kuwa watoto walitembea umbali wa zaidi ya Km 22 kwenda na kurudi shule, wakisoma shule ya sekondari Domel iliyopo Mang'ola Barazani zaidi ya Km 11, hali ambayo ilisababisha watoto wengi kukata tamaa na kuacha shule huku wasichana wakitumbukia kwenye ndoa za utotoni.
Abdala Rashidi ameonesha furaha yake wazi kwa kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwekeza fedha nyingi ambazo zinakamilisha ujenzi wa shule tofauti na hapo awali zililetwa fedha za kujenga darasa moja moja, na kusisitiza kuwa maendeleo ya Serikali ya mama Samia yanakwenda kwa kasi kubwa.
"Haijawahi kutokea kijiji chetu kupata mamilioni ya fedha, huku ni mbali sana lakini mama Samia ametuona na ametuthamini, majengo mazuri kama shule za mjini, watoto wetu sasa hawatasoma mbali, na tutahakikisha wote wanakwenda shule"Amesisistiza Rashidi
Naye Swai Kuzali, amethibitisha kuwa yeye binafsi hakupata nafasi ya kupata elimu ya sekondari, kutokana na mazingira ya shule kuwa mbali sawa na vijana wengine wa kijiji hicho cha Laghangareni na kuahidi kuhakikisha watoto wake wanatumia fursa hiyo kusoma ili kuwa na watalamu kutoka katika kijiji chao.
"Mimi sikusoma sekondari shule ilikuwa mbali, ilitukatisha tamaa, vijana tuliamua kuingia kufanya shughuli za kilimo na uvuvi tunafuraha kwa kuwa watoto wetu watasoma, kijiji chetu kitakuwa na watalamu kama maeneo mengine, Mama Samia kaleta mapinduzi Langhangareni" Amesisitiza Kuzalia
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa shule za sekondari ni utekelezaji wa Ilani yaCCM 2020 kuelekea 2025 Ibara ya 80 kifunga (a) Kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu pamoja na kuhifadhi
na kuendeleza mazingira ya shule hizo
#arushafursalukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.