Rais wa Somalia, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud, ameondoka nchini, jioni ya leo, na kusindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella, kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
Rais huyo wa Somalia, ameondoka nchini, mara baada ya kuhudhuria, Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 23 wa Nchi wanachama za Jumuia ya Afrika Mashariki ( 23rd Ordinary Summit of East Africa Community Head of States), uliofanyika Mkoani Arusha, Ngurdoto Mountain Lorge, wilayani Arumeru.
Mkutano huo wa siku mbili, ulihusisha Wakuu wa Nchi za Wananchama wa Jumuyia za Afrika Mashariki, licha ya mambo mengine yaliyojadiliwa, ulijikita katika kujadili kuhusu masuala ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula, ukitanguliwa na vikao vya ndani na kumalizika leo tarehe 24 Novemba, 2023.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.