Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala mkoa wa Arusha Massaile Albano Musa, ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Meru kujipanga kutumia mapato ya ndani kujenga uzio wa shule ya msingi Leganga eneo la Usa - River pamoja na kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya sekondari Lakitatu.
Ametoa maagizo hayo mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa watumishi wa shule hizo wakati wa kikao cha kusikiliza kero za watumishi, na kuamua kuzitembelea ili kujionea hali halisi, husasani hatari ya wanafunzi kutokana na shule ya Leganga kuwa pembezoni mwa barabara kuu ya Moshi - Arusha, ombi lililotolewa na Mwl. Tajieli Mbwambo, mwalimu shule ya msingi Leganga.
Awali Mwalimu huyo alimuomba katibu Tawala kuona uwezekano wa shule hiyo kuwekewa uzio, kutokana na shule hiyo kuwa karibu na barabara kuu ya Moshi - Arusha, shule ambayo ina kitengo cha wanafunzi wa elimu maalumu huku mwalimu wa shule ya sekondari Lakitatu akiomba kukamilishwa kwa madarasa matatu yaliyojengwa muda mrefu kwa nguvu za wananchi.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Meru, Dkt. Amana Sanga amesema kuwa halmashauri itaangalia uwezekano wa kupata fedha kutoka mapato ya ndani kujenga uzio huo kwa kuwa ni muhimu kwa watoto hao ambao wako kwenye mazingira hatarishi ya pembezomi mwa barabara.
Awali Katibu Tawala mkoa wa Arusha anafanya ziara za kikazi kwenye halmashauri za mkoa huo na kusikiliza kero za watumishi kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuboresha utumishi wa Umma pamoja na utawala bora.
ARUSHA FURSA LUKUKI
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.