Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule Mpya ya Msingi kijiji cha Lemanda kata ya Oldonyosambu, halmashauri ya Arusha na kuagiza kuotesha miti katika maneo yanayozunguka shule ili kuyatunza na kuyahifadhi mazingira hayo.
Katibu Tawala huyo, licha ya kuridhishwa na hatua za utekelezaji wa mradi huo, ameuagiza uongozi wa halmashauri, kufanyia kazi marekebisho madogo madogo yaliyobaki, ili mradi huo ukamilike kwa viwango vya ubora vilivyoainishwa na Serikali.
Amewasisitiza kuotesha miti kwa wingi, ilo kuanza kuyatunza mazingira na kuwafundisha watoto kujenga tabia ya kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka.
"Majengo yameshakamilika, sasa otesheni miti ili kuyatunza na kuyapendezesha mazingira haya, wanafunzi wanatakiwa kujengewa uwezo wa kutunza mazingira, shule ikiwa na miti, ni rahisi kwao kujenga tabia ya kupanda miti hata kwenye maeneo yao tofauti na shule, Ni jukumu lentu kuwafunza wanafunzi kuotesha miti" Amebainisha Missaile.
Aidha amewaagiza viongozi wa vijiji na kata, kuwapa ushirikiano walimu watakaopangiwa kufundisha kwenye shule hiyo ili wawe hutu katika kitekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo, Msimamizi wa mradi huo, amesema kuwa, mradi unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 306.9, fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Ukiwa umejumuisha ujenzi wa jengo la utawala, vyumba vya madarasa 2 vya madarasa ya awali ya mfano, vyumba 7 vya madarasa ya shule ya msingi pamoja na matundu 16 ya vyoo.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.