Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa amekutana na Wamiliki wa vituo binafsi vinavyotoa huduma za Afya Mkoa wa Arusha kwa lengo la kufahamina na kujadili changamoto zinazowakabili katika utoaji huduma hao.
Musa amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika baina yao na serikali katika shughuli zote za utaoji huduma za afya, ili kufikia lengo la serikali za kuhudumia wanannchi.
Amesema kuwa, serikali inatambua na kuthamimi kazi kubwa inayofanywa na watoa huduma za afya, kwa kuwa kazi hizo zinaongeza uwanda wa utoaji huduma kwa wananchi, huduma ambazo zingetolewa na serikali
Aidha amekumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria,,kanuni, taratibu na miongozi ya utoaji huduma zinazotolewa na Serikali ili kutoa huduma bora kwa wananchi zinazozingatia taratibu za uendeshaji wa vituo binafsi za utoaji huduma.
"Serikali na watoa huduma binafsi, wanafanya kazi moja, tunapokutana, licha ya kujadili mustakabali wa huduma za afya kwa jamii, inatupa fursa ya kubaini changamoto zinazokabili sekta ya afya na kupata muafaka wa namna ya kuzitatua kwa pamoja, jambo la muhimi ni kutambua kuwa sote tunalenga kuwahudumia wananchi hivyo ni muhimu kufuata miongozo mbali mbali inayotolewa na serikali"
Awali Wadau hao wametoa changamoto zao juu ya matumizi ya sasa mifumo ya afya, ikiwemo upatikanaji wa leseni pamoja na utoaji wa taarifa kupitia mfumo na kuiomba serikali kuboresha mifumo hiyo ili iwe rahisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Wameweka wazi kuwa mabadiliko ya taratibu ya matumizi ya mifmo katika sekta hiyo, bado mifumo inachangamoto, jambo ambalo linachelewesha utoaji na upatikanji wa huduma kwa haraka ikiwemo upatikanaji wa leseni pindi inapokwisha muda wake.
Hata hivyo kikao kazi hicho kimetoa fursa licha ya kufahamiana na kujadili changamoto, kimetoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuwa na uelewa wa pamoja katila kutoa huduma za afya kwa jamii ndani ya mkoa wa Arusha.
Katika kikao kazi hicho, kimekutanisha zaidi ya wamiliki 200 wa vituo binafsi vya afya na kupanga kuwa vikao hivyo vya mara kwa mara kwa mwaka.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.