Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, Leo jumatatu Februari 03, 2025 ameongoza kikao maalum cha maandalizi ya Sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo yatafanyika Kitaifa Machi 08, 2025 Mkoani Arusha, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kiliwahusisha viongozi mbalimbali wa makundi ya wanawake kutoka Taasisi, Makampuni na vikundi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Arusha.
Aidha, Katibu Tawala huyo amewataka wanawake wote Mkoa wa Arusha Kushiriki katika maadhimisho hayo muhimu yatakayotanguliwa na maonesho mbalimbali kwa vikundi vya wanawake kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo matumizi ya Nishati safi kuanzia tarehe 1-7 Machi, 2024.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.