Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaille Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu, shule ya Sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, mkoa wa Arusha.
Katibu Tawala huyo, licha ya kuupongeza uongozi wa halmashauri hiyo, kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, uliokamilika ukiwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikai
li, ameelekeza mradi huo kuanza kutumika, kwa walimu kuhamia shuleni hapo huku akiwasisitiza kuzingatia utunzaji wa miundombinu ya nyumba hiyo.
Hata hivyo ameipongeza serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwajali walimu, kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya shule sambamba na ujenzi wa nyumba za walimu na kusisitiza kuwa, miundombinu hiyo utarahisishaa tendo la kujifunza na kufundisha.
Akiwasilisha taarifa ya mradi huo, Mkuu wa shule sekondari Kiutu, Mwl. Upendo Lembris, amesema kuwa, Serikali kupitia mpango wa kuboresha Miundombinu ya Elimu Sekondari nchini (SEQUIP), imejengea nyumba ya walimu, yenye sehemu ya kuishi familia mbili (2in1), kwa shilingi milioni 98, shule ya sekondari Kiutu.
Amesema kuwa uwepo wa nyumba hiyo, utawarahisishia walimu kazi ya kufundisha pamoja na kuwapunguzia gharama za kupanga nyumba za watu binafsi huku wakifanya kazi kwa uhuru kwa kuwa muda wote wapo ndani ya eneo la shule
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.