Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi Nasholi, halmashauri ya Meru, leo 29 Novemba, 2023
Mradi huo unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 348.5, fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Mradi unajumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala, vyumba vya madarasa, Madarasa ya awali ya mfano na matundu ya vyoo.
Ikumbukwe kuwa, miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu shule za msingi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, Sura ya tatu Ibara ya 79 kifungu (q)Kukarabati miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na kifungu (C)Kuboresha uratibu na usimamiaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.