Na Elinipa Lupembe
Katibu Tawala mkoa wa Arusha Massaile Albano Musa amewata watumishi kufanyakazi kwa weledi na uadilifu kwa kuzingatia kanuni sheria na taratibu za utumishi wa Umma na kuachana na vitendo viovu ambavyo ni kinyume na maadili ya taratibu za kazi .
Katibu Tawala amesema hayo wakati wa kikao kazi, kilichowakutanisha watumishi wa sekta zote chenye lengo la kusikiliza kero za watumishi sambamba na kuwambushana utekelezaji bora wa majukumu ya kazi katika kuwatumikia wananchi.
Amewasisitiza watumishi kuwa, wanalo jukumu kubwa la kuwahudumia wanachi kwa niaba ya serikali hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, kuwa na nidhamu katika kazi pamoja na kutunza siri za serikali kwa kufuata maelekezo ya viongozi kwa kuzingatia kanununi, sheria, miongozo na taratibu za utumishi wa Umma.
"Fanyenyeni kazi kwa upendo, shirikianeni, heshimianeni kwa kutambua umuhimu wa kila mtu kwa nafasi yake ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita ya kuwahudumia wananchi, serikali imewaamini, rudisheni fadhila kwa wananchi" Amesema Katibu Tawala huyo
Aidha ameutaka uongozi wa halmashauri kuimarisha mahusiano bora kazini kwa kusimamia stahiki na maslahi ya watumishi ikiwemo malipo ya likizo, stahiki za ugonjwa, wastaafu pamoja na malipo ya uhamisho bila kujali nani ni nani.
"Idara ya utawala simamieni Maafisa Watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanafanya vikao na mikutano ya kisheria ngazi za vijiji na kata, kwa kila robo ya mwaka na kuwasilisha mihtasari ya vikao na mikutano ofisi ya mkurugenzi" Amesema
Pia amewataka Maafisa Elimu kata kusimamia vema sekta ya elimu katika shule, licha ya kusimamia taaluma shuleni zaidi kusimamia ulinzi na usalama wa mtoto kuanzia nyumbani mpaka shuleni, upatikanaji wa chakula cha mchana kwa wanfunzi.
Hata hivyo watumishi wa halmashauri ya Arusha wamemshukuru Katibu Tawala kwa kufanya kikao pamoja nao, kikao ambao licha ya kutoa kero zao kimewakumbusha majukumu yao ya kazi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa ili kufikia lengo la serikali la kuwahudumia wananchi.
Afisa Tarafa ya Mukulat Tatu Furaisha, amemshukuru RAS kwa kikao kazi hicho na kubainisha kuwa kiongozi anapokutana na watumishi ni afya katika kazi na kuahidi kufanyia kazi malekezo yote ikiwemo nidhamu ya kazi.
Naye Katibu Tawala Arumeru Joseph Mabiti, ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa hususani katika kata na vijiji kwa kuhakikisha vikao na mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati ili kuongeza uwazi wa shughuli za serikali kwa maendeleo ya wananchi.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amethibistisha kupokea maelekezo na kuendelea kuwasimamia watumishi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na taratibu huku akiahidi kuendela kutoa stahiki za watumishi kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa Umma.
ARUSHA FURSA LUKUKI
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.