Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa, akizungumza kwenye kliniki ya matibabu wakati wa Kambi Maalumj ya Madaktari Bingwa na Wabobezi Mkoa wa Arusha, inayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Juni 24, 2024.
Ikiwa ni siku ya kwanza ya Kampeni ya siku saba iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha chini ya Uongozi shupavu wa Mhe. Paul Christian Makonda @baba_keagan kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya afya maelfu ya wakazi wa mooa huo na mikoa jirani wamejitokeza kuoata huduma hizo za afya zinazotolewa bure.
Awali, Kambi ya Madaktari bingwa ni utekelezaji wa vitendo wa azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kulinda nguvu kazi ya Taifa kwa kuwapatia wananchi huduma bora za afya hususani katika nyanja za uchunguzi wa magonjwa, elimu ya afya kwa Umma na kuimarisha huduma za tiba na kinga kwa jamii.
Lengo la Kambi ya Matibabu haya ni kuwapa wananchi fursa ya kupata elimu ya afya, vipimo vya magonjwa mbalimbali na ushauri wa kitaalam ili kupata huduma stahiki za tiba na kinga ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha inashirikiana na sekta binafsi, Hospitali na Taasisi mbalimbali za Matibabu.
Kaulimbiu ya Kambi hii ya madaktari bingwa inasema "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.