Katibu Tawala Mkoa wa Arusha bwana Missaile Albano Musa leo amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt. Athumani Kihamia.
Katika makabidhiano hayo bwana Albano Musa amesema amekuja kuendeleza kazi ya Serikali iliyokwisha kuanzwa na mtangulizi wake Dkt. Kihamia.
Aidha, amewataka watumishi wa Mkoa wa Arusha kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Nae, Dkt. Kihamia amesema alipata ushirikiano wakutosha kutoka kwa watumishi wote.
Pia, amemuhakikishia Bwana Missaile Musa kuwa changamoto ni zile zile hakuna jipya hivyo anaamini atazimudu.
Katibu Tawala Msaidizi Elimu bwana Abel Ntupwa amesema, kupitia Uongozi wa Dkt. Kihamia ameweza kujifunza mengi ambayo atawafundisha watumishi wengine katika sekta yake ya elimu.
Nae, Katibu Tawala Msaidizi Afya Dkt.Silvia Mamkwe amesema Dkt. Kihamia alijitaidi kuwajali walemavu kwa kuwasaidia katika Uongozi wake, hivyo ni jambo la kuigwa na kila mtu.
Katibu Tawala Msaidizi utawala na rasilimali watu bwana David Lyamongi amemtaja Dkt. Kihamia kama mtu aliyejali watumishi wa ngazi za chini zaidi hasa katika kupata stahiki zao, hivyo wataliendeleza hilo katika kukuza ufanisj wa watumishi.
Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli bwana Rafael Siumbu amesema wao wamejivunia mengi kutoka kwa Dkt. Kihamia hivyo wapo tayari kutoa ushirikiano kwa Katibu Tawala mpya ili kuleta maendeleo kwa Mkoa wa Arusha.
Vilevile, viongozi hao wamemkaribisha Katibu Tawala mpya bwana Missaile Musa na kumuaidi kumpa ushirikiano na kufuata maelekezo yake.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.