RC MAKOND AMASIFU WAZIRI AWESO KWA UCHAPA KAZI WAKE KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CCM
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameridhishwa na utoaji wa huduma ya Maji Mkoani Arusha unaotokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita, na kuahidi kusimamia kikamilifu upatikanaji wa huduma za uhakika za maji zinawafikia wananchi wa mkoa wa Arusha huku akimsifu Waziri wa Maji, Mhe.Juma Aweso kwa uchapakazi wake katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mhe.Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji na miundombinu yake, pamoja na hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma hizoikwa wananchi, mapema leo Oktoba 23, 2024,
Mhe. Makaonda licha kuridhishwa na hali ya upatikanaji wa huduma za maji Jiji la Arusha unaokwenda takribani 90% na saa 23 kwa siku, amempongeza pia Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kwa umahiri wake, katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kupeleka huduma ya maji kwa wananchi kote nchini Tanzania.
Katika hatua nyingine Mhe. Makonda amezitaka mamlaka za Maji mkoani Arusha kuja na mkakati maalum wa kusaidia wananchi wasiokuwa na uwezo, kwa kuwaunganishia huduma ya maji na kuwa na mpango wa ulipaji wa gharama za kuunganishiwa huduma ya maji kwa awamu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.