Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameagiza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Dola kwaajili ya mahojiano watu wote wanaotuhumiwa kuiba kiasi cha Shilingi Milioni 252, zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya manunuzi ya eneo la ekari sita zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa shule kwenye Kata ya Murieth Jijini Arusha.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha leo Jumatatu Februari 24, 2025, Mhe. Makonda amesisitiza tena umuhimu wa Viongozi kuhudhuria vikao vinavyowahusu, akilaani tabia ya kutohudhuria vikao na kuzungumza kwenye mikutano ya hadhara yale yanayopaswa kuzungumzwa, kujadiliwa na kutafutiwa majibu ndani ya Vikao.
Kulingana na taarifa mbalimbali mtandaoni, inaelezwa kuwa Wizi huo unadaiwa kutaka kutekelezwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya jiji la Arusha, baada ya kudai kuwa Shilingi Milioni 552 zilitakiwa kulipwa katika ununuzi wa eneo hilo la ujenzi wa shule kata ya Murieth badala ya thamani halisi ya eneo hilo ambayo ilikuwa ni Shilingi Milioni 300 za Kitanzania.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.