Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameagiza kupewa kipaumbele kwa Viongozi wa dini na Wazee wote wa Mkoa wa Arusha pale watakapokuwa kwenye Ofisi zote za Umma Mkoani Arusha kwaajili ya kutafuta huduma ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi na kudumisha Upendo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kundi hilo muhimu kwa amani ya nchi.
Mbele ya waumini wa Msikiti Mkuu wa Bondeni Jijini Arusha Ijumaa Oktoba 25, 2024, Mhe. Makonda amesema kutokana na umuhimu wa watu hao, hawatakiwi kupanga foleni kwenye kutafuta huduma za umma akitaka waenziwe kwa mchango wao katika amani ya Tanzania, akiagiza pia Wasaidizi wake kuwa na utamaduni wa kuwatembelea mara kwa mara ili kuwasikiliza na kutatua changamoto walizonazo.
Katika Hatua Nyingine Mhe. Paul Christian Makonda ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kumuombea Kheri Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutokana na Upendo wake mkubwa na dhamira njema aliyonayo kwa Watanzania wote.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.