Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali mpya ya wilaya ya Karatu, iliyoko kijiji cha Changarawe Kata ya Daa Tarafa ya Karatu huku tayari imeanza kutoa huduma tangu Januari 23, 2024.
Akizungumza na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Victor Kamazima pamoja na viongozi wengine hospitalini hapo, RC Makonda amehimiza kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na Taasisi mbalimbali za kidini zilizotoa mchango mkubwa katika sekta zoye hasa sekta ya Afya.
" Zipo Taasisi za dini zilizotoa mchango mkubwa kwenye sekta mbalimbali hususani kwenye sekta ya Afya, kujenga kwetu hospitali tusiwe na kiburi cha kuwadharau, tengenezeni mahusiano mazuri ili hata mkiwa na changamoto mkaweza kusaidiwa au nyie kuwasaidia ikiwa ni lengo la Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwasaidia watanzania katika kila sekta hasa Afya kwakuwa ndio inabeba uhai wa mwanadamu". Amesema Mhe. Makonda
Hata hivyo, amepokea kilio cha upungufu wa dawa ambapo alimtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amani, kutolea majibu ambapo alisema changamoto hiyo ipo japo si kwa ukubwa lakini wamekuwa wakiendelea kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha.
Sambamba na hilo, RC Makonda alipokea changamoto ya kutokuwepo kwa umeme wa ziada iliyotolewa na mmoja kati ya mwananchi ambapo kwa majibu ya Dkt. Amani alisema tayari wameshanunua jenereta la ziada kwaajili ya kuepukana na changamoto ya umeme pale ambapo ikitokea umekatika.
Akitolea majibu kuhusu malalamiko ya ufinyu wa muda wa kuwaona wagonjwa, RC Makonda ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kutumia busara katika kukabiliana na changamoto hiyo ilikusudi wananchi wanaokuja kuona wagonjwa wao na wao wapate faraja.
"Kila pahala kuna utaratib wake lakiniwakati mwingine tumieni busara ya kutazama mazingira yenu yapoje kwa maana ya upatikanaji wausafiri na umbali na watu wengine hawana uwezi wa kulipia hoteli za karibu na hapa kwakuwa kama mnavyojua Arusha ni Mji wa kitalii gharama zake za hoteli kiasi zinakuwa juu"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.