Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amesikitishwa na tuhuma za rushwa zinazoukabili mkoa huo na kujipanga kuongeza kikosi kazi kitakachoongeza nguvu ya mapambano ya rushwa mkoani humo.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara wa kuzungumza na wananchi wa halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru ikiwa ni siku ya nnne ziara yake ya 'Siku 6 za Moto Arusha' ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi ili kusikiliza kero.
Amesema kuwa, ili kukabiliana na mafisadi na wala rushwa mkoa huo unahitaji Taasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa nchi TAKUKURU kukiongezea nguvu kikosi cha Arusha pamoja na kumuomba Mkaguzi Mkuu na Mdhitbiti wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi upya katika eneo la mapato na matulizi pamoja na fedha za utekezaji wa miradi ya maendeleo.
Ameweka wazi kuwa, mkoa unahitaji kufanya mambo mawili, ambapo ameyataja kuwa ni pamoja na moja ni kumuomba Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Tanzania TAKUKURU · CP. Salum Hamduni kuongeza kikosi kazi cha TAKUKURU maalum kwa kufanyakazi kwenye mkoa wa Arusha, ili kupambana na Rushwa, nataka tusafishe Mafisadi na wala rushwa wote kwa kuwa kazi tuliyonayo sasa tunaelemewa, tunahitaji kikosi kikubwa zaidi, ili mkoa wa Arusha uwe wa mfano
"La pili tutamuomba Mkaguzi Mkuu na Mdhitbiti wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi upya 'auditing' kuanzia kwenye vyanzo vya mapato mpaka kwenye matumizi yote ikiwemo ulipaji wa fedha za utekelezaji wa miradi"
"Leo nimegoma kusaini barua ya Jiji la Arusha, ambao walijipima na kuona wanauwezo wa kukusanya mapato mpaka bilioni 60, wakashusha mpaka bilioni 48, leo wanaomba nisaini barua kushusha mpaka bilioni 42, ninafahamu mtandao huu si mdogo, uko uwezekano wa watumishi wa juu walio nje ya huu mkoa, wanapunguza vigezo na makubaliano yaliyopitishwa na Baraza la Madiwani, wanashusha vyanzo ili wapate fursa ya kujipatia pesa hizo"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.