Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa, Mhe.Paul Christian Makonda akikagua gwaride la heshima la Jeshi la Polisi Tanzania, wakati alipofika kwenye Kikosi cha Kutuliza ghasia - FFU - Oljoro jijini Arusha mapema leo Mei 31, 2024.
Mhe. Makonda amefika kwenye kikosi hicho kwa ajili ya kukabidhi pikipiki 50 na gari moja kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ikiwa ni mkakati wa mkuu wa mkoa huyo wa kuhakikisha jeshi hilo linakuwa na vitendea kazi vya kutosha kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mkoa huo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.