Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekagua Helkopta maalumu ya wagonjwa, iliyoandaliwa kwaajili ya huduma za dharura kwa wagonjwa watakaokuwa na uhitaji wa kusafirishwa kupelekwa kwenye Hospitali mbalimbali za rufaa kwaajili ya Matibabu ya zaidi.
Mhe. Makonda amepanda helkopta hiyo, ikiwa ni sehemu ya kujiridhisha na huduma hiyo, muda mfupi baad aya kuzindua Kambi Matibabu ya Madaktari Bingwa na Wabobezi itakayofanyika kwa siku saba kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abedi Jijini Arusha, iliyoanza leo Juni 24, 2024
Kambi hiyo imehusisha Madaktari Bingwa na wabobezi pamoja na wahudumu wa afya zaidi ya 450 yenye Kaulimbiu ya "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.