Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Monduli leo Mei 27, 2024.
Katika mradi huo, Mhe. Makonda ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi zilizoweza kutekeleza miradi ya maendeleo kisekta ikiwemo fedha za upanuzi wa majengo muhimu kwenye hospitali ya wilaya ya Monduli, majengo ambayo yanakwenda kukamilisha na kuipa hadhi ya hospitali ya wilaya hiyo pamoja na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma za afya ndani ya eneo lao.
" Tunaamini mwishoni mwa mwezi Juni majengo yatakuwa yamekamilika na kuanza kutoa huduma, ninawasisitiza endeleeni kurekebisha changamoto zote zilizoainishwa na timu zilizotangulia na mimi, wakati mwingine nikija hapa nikute majengo yenye viwango vya ubora kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa" Amesisitiza
Aidha, amekitaka Kitengo cha Ustawi wa Jamii kufanya kazi vizuri ya kuhudumia wananchi wenye changamoto ili kuhakikisha wanazishughulikia kero zote na kuhakikisha zinaishia hapa bila ya kufika mkoani.
"Rai yangu kwa watendaji na waandisi mnapojenga maje go zingatieni mahitaji yote ya majengo ikiwemo maneneo ya kuingiza hewa na zima moto".Amesema Mhe. Makonda
Hata hivy Mhe. Makonda ameuagiza uongozi wa wilaya hiyo kusimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, 2024 na majengo hayo yaweze kutumikia kuwahudumia wananchi kama yalivyo makusudi ya serikali ya awamu ya sita.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.