RC MAKONDA AKAGUA UKARABATI WA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID IKIWA NI MAANDALIZI YA MEI MOSI KITAIFA 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ametembelea na kukagua maendeleo ya marekebisho ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku kuu ya wafanyakazi Duniani, inayotarajiwa kufanyika tarehe 01.05. 2024.
Mgeni wa Heshima katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tumaini Nyamhokya Rais wa Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini Tanzania pamoja na Makamu mwenyekiti wake na wakuu wengine wa idara mbalimbali waliambatana na Mhe. Makonda kwenye ukaguzi huo wa maandalizi ya sherehe hizo kubwa kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali.
Hata hiyo, Nyamhokya ameviambia amebqinisha kuwa, maandalizi yanaendelea vyema na kila kamati inafanya kazi yake kikamilifu ili kuhakikisha kuwa sherehe hizo zinakuwa nzuri na za kuvutia.
Amefafanua kuwa, kufanyika kwa shughuli hiyo mkoani Arusha ni fursa pia kwa wakazi wa Arusha na wageni mbalimbali kwani watapata fursa za kuuza bidhaa mbalimbali za vyakula, vinywaji na sehemu za kulala wageni watakaohudhuria maadhimisho hayo kwa mwaka huu ambapo tayari baadhi ya wageni wamekwishaanza kuwasili mkoani hapa.
Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani ni siku ya mshikamano kwa Wafanyakazi wa sekta zote katika kusimamia na kuunga mkono Haki, Wajibu na Dhamana ya wafanyakazi kote ulimwenguni katika mchakato wa kufikia maendeleo endelevu.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.