Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekagua Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni hatua za mwisho za maandalizi ya sherehe ya kuelekea sikukui za Mei Mosi, zinazofanyika Kitaifa Mkoani Arusha, Mei 1, 2024
Akiwa uwanjani hapo Mhe. Makonda, ameshuhudia fainali za michezo mbalimbali ya wafanyakazi kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za sherehe hizo za wafanyakazi duniani zinazotarajiwa kufanyika Mei Mosi.
Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye anayetarajiwa kuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zenye nia ya kujadili changamoto na mafanikio ya wafanyakazi, kutambua na kuwapongeza wafanyakazi kwa utumishi wao kwa Jamii.
Kwenye ukaguzi huo wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mhe. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Bw. Missaile Musa, Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Justine Masejo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.