Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Februari 24, 2025 amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ubelgiji kwenye shirika la Chakula na kilimo duniani FAO Mhe. Levien De La Marche na Balozi wa Switzerland kwenye Umoja wa Mataifa Mhe. Kristztina Bende, ambao wameambatana na Maafisa waandamizi wa shirika hilo la Chakula, wakiwa Mkoani Arusha kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo Wilayani Monduli na Karatu.
Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine, Mhe. Makonda amewasilisha maombi yake ya kuwaomba Mabalozi hao kuwa Mabalozi wa kuvutia Uwekezaji Mkoani Arusha kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya matibabu, akiwahakikishia usalama, Mazingira bora ya uwekezaji pamoja na ushirikiano wa kutosha kutoka kwenye Ofisi yake katika kuhakikisha kuwa uwekezaji wao unakuwa wa manufaa.
Mhe. Makonda amewaeleza kuhusu jitihada mbalimbali za kuimarisha ulinzi na usalama kwenye Mkoa wa Arusha tangu kuteuliwa kwake kuongoza Mkoa huo, akisema tamanio la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona kila mtu anakuwa huru kufanya shughuli zake halali, kutumia fursa zilizopo Mkoani humo pamoja na kuwa na mchango katika uchumi na uzalishaji wa ajira mpya kwa Vijana.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.