Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekerwa na tabia ya malumbano na kuvutana kwa viongozi, Baraza la Madiwania na Watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, suala ambalo linasababisha kukwama kwa utekelezaji wa shughuli za ikiwemo ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo licha ya Serikali Kuu kutoa fedha za kutekeleza miradi hiyo kisekta.
Mhe. Makonda akemea tabia hiyo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Jiji la Arusha, mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa wilaya hiyo, iliyowasilishwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Felician Mtahengerwa, taatifa iliyobainisha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo kutokana na mabishano, malumbano na kutokuelewana kati ya Menejimenti ya Jiji la Arusha, Baraza la Waheshimiwa Madiwani na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini.
Mhe.Mtahengerwa, amemueleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, migongano mwa changamoto zinazokwamisha maendeleo ya Jiji la Arusha ni pamoja na kutokuelewana kati ya viongozi wa kuteuliwa, wa kuchaguliwa na Watendaji, jambo ambalo linasababisha adhabu kubwa kwa wananchi kutokana na miradi muhimu kukwama na hivyo kuwachelewesha kimaendeleo.
Hata hivyo, Mhe. Makonda ameweka wazi hisia zake kwa viongozi hao kuwa, ingekuwa ni mamlaka yake angeivunja Mamlaka hiyo ya Jiji la Arusha, huku akihoji umuhimu wa Jiji kuwepo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Arusha.
Kufuatia hali hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amelitaka pia Baraza la Madiwani Jiji la Arusha kujitafakari na kuamua kuwa sauti ya wananchi kikamilifu na kupambana ili kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana kwa kukamilisha miradi yote ya maendeleo kwa wakati.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.