Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na kufanya kikao kazi maalum na Maafisa wa Mamlaka za maji Mkoa wa Arusha, Mamlaka ya Maji safi ja Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha na Mamlaka za Maji mijini na Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Arusha, leo Agosti 17, 2024.
Kikao kazi hicho kimefanyika kwenye Ofisi kuuu za Mamlaka ya Maji AUWSA eneo la Mateves, chenye lengo la kujadili kuhusu hali ya upatikanaji wa majisafi, ya uhakika na salama mkoani Arusha na namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye upatikanaji wa majisafi ya uhakika mkoani Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.