Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuimarisha kikosi chake cha Intelijensia ili kuzuia na kukabilina na uhalifu mkoani hapo.
Ametoa agizo hilo wakati wa akikabidhi Pikipiki 50 na gari moja kwa pamoja vyenye thamani ya shilingi ya takribani milioni 205 kwa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, kwa kusisitiza Jeshi hilo kuimarisha kitengo chao cha Intelejensia ili kuhakikisha wanapata taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu kabla ya haujatokea, kuwa na uwezo wa kukabiliana nao kwa wakati pindi unapotokea pamoja na kutoa taarifa ya matokeo ya uhalifu na wahalifu kwa jamii.
"Kikosi cha Intelijensia kikiwa imara na makini, kitakuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia uhalifu lakini zaidi kuwa na taarifa zitakazowezesha kukabiliana na uhalifu pindi unapotekea jambo ambalo litawapa wananchi imani na Jeshi lao la Polisi badala ya kuendelea kulitupia lawama, niombe pia muwe na tabia ya kutoa mrejesho kwa jamii ya namna mlivyokabiliana na uhalifu uliotokea". Amesisitiza
Aidha, Mhe. Makonda ameweka wazi kuwa, ni vyema Jeshi hilo la Polisi kujikita katika kukabiliana na uhalifu kabla haujatokea kwa kuwaruhusu kudhibiti na kukabiliana na uhalifu na wahalifu kabla ya kutekeleza matukio.
Kadhalika Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka Askari Polisi Mkoani Arusha kuwa waadilifu na waaminifu katika majukumu yao na kujiepusha na ukandamizaji wa haki na upokeaji wa rushwa ili kujenga uaminifu kwa Jamii inayotakiwa kushirikiana nao katika ulinzi na usalama wa Mkoa wa Arusha.
Mhe.Makonda amebainisha kuwa, usalama ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtaka kuimarisha Utalii huku akisisitiza kuwa kivuti kikuu cha watalii na wageni wanaofika Arusha ni usalama na utulivu wa maeneo yote katika mkoa huo.
Awali, pikipiki hizo 50 na gari moja aina ya Fortuner vimetolewa na Benki ya CRDB na NMB pamoja, kampuni ya vifaa vya umeme ya MCL kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa katika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mkoa wa Arusha.
#ArushaNaUtalii
#KaziIendelee
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.