Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akisalimiana na Familia ya Baba Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Jacob Massangwa ambaye leo Jumapili Septemba 29, 2024 Jijini Arusha kwenye Usharika wa Kimandolu, amestaafishwa kwa heshima na kanisa la KKKT baada ya kuhudumu Kanisani tangu mwaka 1982.
Usharika wa Kimandolu Mkoani Arusha unamshukuru na Kumtaja Askofu Solomon kwa kuhamasisha kulipa madeni ya kanisa, Kuongeza fursa za elimu kwa wachungaji wapya, Kuboresha ibada kwa Kuongeza wataalamu wa Muziki kwenye Dayosisi na kuongeza uinjilishaji kwenye majimbo ya Maasai kusini na Kaskazini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.