Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuujali mkoa wa Arusha huku akiungalia kwa jicho la kipekee, na kuwezesha miradi mingi ya maendeleo mkoani humo, kutoka na malengo ya kuimarisha sekta ya Utilii, sekta inayoingiza fedha nyingi za kigeni nchini.
Mhe. Makonda, ametoa shukurani hizo, wakati akizindua magari mawili na kukabidhi kwa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha, hafla iliyofanyika kwenye Ofisi kuu za Jeshi hilo, mapema leo Mei 20, 2024.
Amebainisha kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia, inafanya kazi kubwa ya kupeleka maendeleo karibu na wananchi kona zote nchini huku mkoa wa Arusha ukinufaika zaidi katika sekta zote ikiwemo kuimarisha zaidi, eneo la ulinzi na usalama wa mkoa huo.
Mhe. Makonda amekiri kuwa, katika kuimarisha usalama wa mkoa wa Arusha, Mhe. Rais ametoa magari 2 kati ya magari 12 yaliyogawiwa nchi nzima, magari ambayo ni mapya na ya kisasa ili kuwezesha utendaji kazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, yanakwenda kuimarisha usalama wananachi na mali zao katika mkoa huo.
"Tumepewa magari mawili kwa Jeshi letu la Zimamoto na Uokoaji na kufanya mkoa kuwa na magari 6 sasa, kila mmoja ni shahidi wa jitihada kubwa za Dkt.Samia za kuhakikisha mkoa wa Arusha unakua katika sekta zote, kwa miaka mitatu ametoa takribani trilioni 1.8 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kisekta lakini zaidi anawekeza nguvu kubwa katika kuimarisha sekta ya Utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa la Tanzania" Amesema Mhe. Makonda
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, kwa kuwa asilimia 80 ya Uchumi wa mkoa huo, unategemea wageni wa ndani na nje ya nchi ambao wanafika kwa ajili ya shuguli za kikazi na zaidi utalii, shughuli ambazo zinahitaji usalama wa uhakika wa watu na mali zao.
Awali, Mhe. Makonda amezindua magari hayo ya kisasa yaliyotolewa na Serikali ya awamu ya sita, kwa ajili ya shughuli za kuzima moto na ukoaji, yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 1.9.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.