Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatano Novemba 27, 2024 ameungana na Watanzania wengine kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye kituo alichokuwa amejiandikishia cha Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama Kata ya Sekei Jijini Arusha.
Mara baada ya kupiga kura asubuhi hii, Mhe. Makonda akizungumza na wanahabari amewasihi wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye Uchaguzi huo kwani ndiyo sehemu pekee inayompa uhuru na mamlaka mwananchi mwenye sifa katika kuchagua na kuunda serikali aitakayo.
Katika hatua nyingine Mhe. Makonda pia amewataka wananchi mara baada ya kupiga kura kuondoka vituoni na kuachana na jukumu la kutaka kulinda Kura kwani jukumu hilo kulingana na sheria na taratibu za uchaguzi huo linabebwa na Mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo muhimu kwa maendeleo ya Mitaa na Vijiji.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.