Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesisitiza umuhimu wa Wananchi wa Arusha kuendelea kuitunza Amani iliyopo Tanzania kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa letu.
Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 15, 2024 mara baada ya kupokea Ujumbe maalum ulioongozana na Mwenge wa Uhuru wakati wakiwa njiani kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kuupandisha mwenge huo Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya sherehe ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za Mwenge huo.
Kupandishwa kwa Mwenge huo Mlima Kilimanjaro kunakofanywa na maafisa wa Jeshi la wananchi JWTZ ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo tukio hilo si tukio la kawaida bali lina maana kubwa kwa taifa, ikiakisi ujumbe wa maendeleo, amani pamoja na mshikamano kwa Taifa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.