Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda ametembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yaliyoathirika na maji, yaliyotokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wakati wa mvua pamoja na kuhama katika maeneo yenye historia ya kuwa na mikondo ya maji.
Amesema kuwa, kufuatia Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania, kutakuwa na mvua kubwa zitakazonyesha kwenye mikoa mingi nchini, hivho kila mwananchi anatakiwa kuchukua tahadhari ya mvua hizo ikiwemo maderava wa vyombo vya moto ili kupunguza hasara na watu kupoteza maisha.
"Niwatake watu wanaoishi kwenye maeneo yenye historia ya mikondo ya maji kuchukua tahadhari kubwa kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha, lakini zaidi kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto, uwakati wa mvua kubwa ni vema kusubiri na pindi ukiona mvua usivuke na gari wala bodaboda, hii itapunguza madhara yanayoweza kutokea bila sababu za msingi" RC Makonda
Hata hivyo, wananchi wa maeneo hayo wamemuelezea Mkuu wa mkoa huyo namna ujenzi wa Barabara ya Mianzini kuelekea Timbolo usiokamilika kwa muda mrefu sasa, ujenzi ambao umekuwa kero kwa wananchi hao, hasa msimu wa mvua, kutokana na kuwa barabata hiyi ni asili ya mkondo wa maji suala ambalo linatatiza usafiri na usafirishaji.
Aidha, Wananchi na wafanyabiashara wenye maduka pembezoni mwa barabara hiyo wameiomba Serikali kuharakisha kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo ya Mianzini - Timbolo na kuomba kuangalia namna ya kuongezwa kwa vipenyo kwenye Mto Ngarenaro na daraja la Mula ili kuruhusu upitishaji wa maji mengi kwa wakati mmoja, kwa kuwa sasa madaraja hayo yanazidiwa na wingi wa maji.
"Tunaiomba Serikali kuweka mifereji pembezoni mwa barabara zote, ili kudhibiti uharibifu wa barabara wakati mvua kubwa zinaponyesha, barabara nyingi hazina mifereji pembezoni, jambo ambalo linasababisha maji kupita juu ya barabara na mengine kuingia kwenye makazi ya watu, sasa licha ya kuharibu barabara yanaharibu nyumba, mali za watu na kusababisha hasara kubwa na wakati mwingine vifo vya watu, tunakuomba Mheshimiwa Mkuu wa mkoa kuangalia upya suala hili" Wananchi
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.