Mradi huu unatokana na mahusiano mazuri ya Tanzania na Falme za kiarabu_
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Ndugu Mussa Misaile na viongozi wengine wa serikali ya Mkoa na Wilaya ya Ngorongoro wametembelea na kukagua mradi mkubwa wa uchimbaji wa visima virefu vya maji vinavyochimbwa wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mradi huo mkubwa wa maji unatekelezwa kwa pamoja na serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai inayoongozwa na Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum, mtawala wa Dubai ,bilionea na makamu wa Rais wa milki za kiarabu UAE ukiwa na malengo ya kuchimba visima virefu 37.
"Leo tunakuja kuwaambia kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwanadiplomasia namba moja, Mkuu wa nchi yetu na Rais wetu ametujengea mahusiano mazuri na nchi za Falme za kiarabu na sisi wana Ngorongoro tumeanza kuyaona matunda hayo ikiwa ni ndoto na shauku ya Makamu wa Rais Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.", amesema Mhe. Makonda.
Kulingana na taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, hadi sasa jumla ya visima 18 vimeshachimbwa kwenye vijiji mbalimbali, ambapo visima 12 kwenye vijiji vya Oloboo, Maaloni, Wasso na Siteti vimeshakamilika na wananchi wameanza kunufaika kikamilifu na mradi huo mkubwa wa maji.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.