Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, amejitokeza kutoa pole kwa familia ya Wilson Lengima, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli, kufuatia msiba wa mama yake mzazi aliyefariki dunia hivi karibuni.
Mheshimiwa Makonda ameongoza ujumbe wa viongozi mbalimbali wa serikali na chama, kuifariji familia ya marehemu pamoja na wananchi wa eneo hilo.
“Tumekuja hapa kuungana na familia ya ndugu yetu Wilson Lengima katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu na tunamuomba Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.” Amesema.
Mama mzazi wa Wilson Lengima amezikwa kijijini kwao Losimingori, ambapo mamia ya waombolezaji wamekusanyika kwa ajili ya ibada ya mazishi na kutoa heshima zao za mwisho.
Viongozi wa chama na Serikali wameendelea kusisitiza mshikamano na kutoa pole kwa familia ya Lengima, huku wakiwahimiza wananchi kuendelea kuwa na subira na mshikamano katika nyakati hizi za majonzi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.