Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda amemuomba Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango kumfikisha salamu za wananchi wa Arusha kwa Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa, wananchi wa Arusha wanatambua mchango wake hasa kwenye sekta ya utalii, kupitia programu ya Tanzania The Royal Tour.
Mhe. Makonda ametuma salamu hizo, wakati akitoa salamu za mkoa huo kwenye sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani - Mei mosi, zinazofanyika kitaifa Mkoani Arusha kwenye, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mei 01.2024
Amesema kuwa, programu hiyo ya Roayal Tour imeleta manufaa makubwa kwa kuwa tayari imeanza kuzaa matunda yanayowanufaisha licha ya kuwawezesha wakazi wa Arusha kujipatia kipato, imeongeza uchumi na Taifa kwa ujumla wake.
Mhe. Makamu wa Rais, nikuombe utufikishie salamu kwa Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba programu ya Royal Tour imetunufaisha sana wananchi wa kila kada awe ni muuza mchicha, awe ni Bodaboda, awe ni mtu anayelima nyanya, Bilinganya n.k, anafaidika na Utalii kwa kuwa Hoteli zikijaa na yeye anapata nafasi ya kuuza bidhaa na huduma na hatimaye anamudu kuendesha maisha yake". Ameweka wazi Mhe. Makonda
Ameongeza kuwa, wananchi wa jiji la Arusha na mkoa wa Arusha kwa ujumla wake wanayo furaha kubwa sana, kwa kazi kubwa aliyoifanya ya katika sekta ya Utalii, 'Royal Tour', tunapoelekea msimu wa Utalii 'high season' tunategemea kupata watalii wengi wa ndani na nje ya Nchi.
Hata hivyo Mhe. Makonda amemuhakikishia Mhe. Rais kuwa Arusha ipo salama huku akisisitiza anga la Arusha lipo mikono salama ya Menyenzi Mungu @baba_keagan
Kauli mbiu : "Nyongeza ya Mshahara ni Msingi Bora na Kinga ya Hali Ngumu ya Maisha" @ikulu_mawasiliano
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.