Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amewaalika wananchi wa Mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kuungana na Wafanyakaizi wote nchini kushiriki kwenye sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi itakayofanyika tarehe 01.5.2024 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mhe. Makonda amesema hayo, wakati akimkaribisha NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana na wenye Ulemavu, kufungua kikao cha kamati ya maandalizi ya Mei Mosi 2024, kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Aprili 20, 2024
Amesemq kuwa, wananchi wanatambua mchango wa wafanyakazi nchi katika utaji wa huduma kisekta, hivyo kwa umuhimu huo, amewaalika wananchi wote kuungana na wafanyakazi wote nchi kufurahia kwa pamoja mafanikio ya wafanyakazi kwa kusherehekea siku hiyo muhimu ya Mei Mosi Kitaifa inayofanyika mkoani Arusha Kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
"Ni bahati iliyoje kupata upendeleo Mei Mosi kufanyiaka Arusha, nitumie fursa hii kuwaalika rasmi ndugu zangu wanaarusha kushiriki kwenye sikukuu ya Mei Mosi ambapo Rais wetu Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi, kila mmoja kwa nafasi yake ninaomba ashiriki tukio hilo muhimu kwa mkoa wetu wa Arusha"Amesisitiza Mhe. Makonda
Aidha, amewataka wakazi wa Arusha, kuwapokea wageni wanaofika Arusha kwa shughuli hizo za Mei Mosi na kuwapa ushirikiano pamoja na kutumia fursa hiyo kuwakarimu katika maeneo yote ya biashara ambayo ugeni huo mkubwa utahitaji huduma.
"Nafahamu watu wa Arusha ni wakarimu, wahudumieni vizuri wageni wote na kuhakikisha wanapata hudumq bora ili wafurahie kuwepo Arusha, fursa ambayo inakuza uchumi wa mkoa wetu" Amesema
Awali, kikao hicho kimejumuisha wanakamati , viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wakioongozwa na rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, sekretarieti ya mkoa wa Arusha viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Missaile Musa pamoja na Makamishna wa Kazi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.