Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ameongoza maelfu ya wakazi wa Mkoa wa huo kuwaombea Kheri manusura wa ajali ya kuporomoka kwa Jengo la Ghorofa nne, ajali iliyotokea jana Novemba 16,2024 katika makutano ya Mtaa wa Congo na Mchikichi, Kariakoo Jijini Dar Es salaam.
Mhe. Makonda amewatakia kheri manusura wa ajali hiyo, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wake na waandishi wa habari wa Ripoti ya mafanikio ya Serikali mkoa wa Arusha kwa kipindi cha cha miezi ya uongozi wake mkoani Arusha, mkutano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimayaifa (AICC) ukumbi wa Simba, leo Jumapili Novemba 17, 2024.
Kulingana na Mrakibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dar Es salaam Bw. Peter Mtui amewaambia wanahabari kuwa watu watano wamefariki dunia katika ajali hiyo, huku wengine 45 wakijeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya Jumamosi ya Novemba 16, 2024 na mpaka hivi sasa jitihada mbalimbali za uokozi zinaendelea.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.