Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.Paul Christian Makonda amewasili wilayani Monduli na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Mhe. Festo Shemu Kiswaga mapema leo Mei 27, 2024.
Licha ya kusaini kitabu cha wageni, Mhe. Makonda amepokea taarifa ya wilaya hiyo pamoja na kuzungumza na viongozi, Kamati ya usalama wilaya pamoja na watumishi wa wilaya hiyo.
Mhe. Makonda yupo wilayani Monduli ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku sita maarufu kama 'Siku 6 za Moto Arusha' ya kukagua shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara.
Akiwa wilayani Monduli, Mhe. Makonda atakagua anatembelea na kukagua mradi wa upanuzi wa hospitali ya wilaya, mradi wa maji kijiji cha NAFCO pamoja na Kufanya Mkutano wa Hadhara Meserani eneo la Duka Bovu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.