Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda @baba_keagan amezungumza na wananchi walioikafika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kupata huduma za maibabu zinazoolewa bure kwenye Kambi ya siku saba ya Madaktari Bingwa na Mabingwa Wabobezi Arusha na kuwasisitizatata tamaa ya kutibiwa kutokana na idadi kubwa ya watu badala yake kuwa wavumilivu kwa kuwa Serikali imejipanga kuwahudumia watu wote waliofika kupata huduma za afya pamoja na kuandaa utaratibu wa kuwahudumia kwa makundi
"Ninawatangazia wananchi wote tumeandaa utaratibu mpya wa kuhudumia kwa kuzingatia uwepo wa watu wa makundi maalum ya wazee, watoto na aki mama wajawazito, wagonjwa mahututi ili kuwaepusha kukaa muda mrefu kwenye misururu" Amesema
Aidha, ametangaza kuongezeka kwa madaktari wengine 100 na kufikia wahudumu wa afya 550 kutoka idadi ya wahudumu wa afya na madaktari 450 waliokuepo hapo awali, na kusiitiza kuwa lengo ni kuongeza kasi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wenye uhitaji wa matibabu, vipimo pamoja na dawa.
Kaulimbiu ya Kambi hii ya madaktari bingwa ni "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.