Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Rc Paul akiwa kwenye Paredi ya magari chapa ya Land Rover, wakati ya tamasha la Land Rover Festival 2024, ililofanyika mkoani humo Oktoba 12, 2024.
Takribani magari 1,034 aina ya LandRover yamekusanyika na kushiriki Paredi hiyo na kutembea umbali mrefu wa Kilomita 14 kutoka King'ori wilaya ya Arumeru mpaka uwanja wa Magereza Kisongo Jijini Arusha.
Arusha Land Rover Festival 2024, imevunja rekodi ya Dunia kwa kuyakutanisha magari mengi zaidi, ikilinganishwa na Tamasha la magari aina ya Land Rover liliyofanyika Nchini Ujerumani mwaka 2018, ambapo jumla ya magari 632 yalikusanyika kwa pamoja na kutembea umbali wa Kilomita 7.4 pekee, rekodi iliyoandikwa kwenye kitabu cha 'Guinness Book'
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.