• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RC MONGELLA AAGA KUNDI KUBWA LENYE KAYA 118 KUPISHA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO

Posted on: January 25th, 2024


Na Elinipa Lupembe.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, ameliaga kundi la nne awamu ya pili, lenye jumla ya kaya 118 na watu 818, kundi ambalo ni kubwa kuondoka kwa hiari, kutoka kwenye eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, zikielekea maeneo ya Msomera Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, Kitwai Wilaya ya Simanjiro na Saunyi Wilaya ya Kilindi na maeneo mengine waliyoyachagua wenyewe.


Akizungumza wakati wa zoezi la kuwaaga wananchi hao, wakiwa na mifugo yao 3,129, Mhe. Mongella amewapongeza kwa uzalendo mkubwa, waliouonyesha kwa nchi yao, kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa, bila kujali masilahi yao binafsi huku akiwahakikishia usalama wa maisha yao, kiuchumi na kijamii pamoja na kulipwa haki zao zilizoainishwa kisheri.


Ameongeza kuwa, pamoja na mikakati wa Serikali, kuendelea kutunza eneo la hifadhi ambalo ni Urithi wa Dunia, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuhakikisha Serikali inasimamia ulipwaji wa haki za msingi za wananchi walioamua kuhama kwa hiari kupisha eneo hilo.


"Dkt. Samia amehakikisha kila Kaya inayokwenda Msomera na maeneo mengine, inapata nyumba kwa ajili ya makazi, eneo la kilimo na mifugo pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya, maji, umeme, shule ili kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule" Ameweka wazi Mhe. Mongella.


Awali, Mhe. Mongella ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajafanya maamuzi ya kuhama eneo la hifadhi, kufanya maamuzi kwa haraka, kwa kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha wananchi hao, wanapata haki zao zote kwa wakati na kuwataka Maafisa Wahifadhi kuendelea kutoa  elimu ili waweze kuhama kwa hiari.


Hata hivyo, wananchi hao wameishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa uongozi makini wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu, kwa kuwajali na kuamua kuwahamisha eneo la Hifadhi, ambalo lilikuwa ni hatarishi kwa maisha yao pia.


Sindato Ngenyike Mollel,  aliyekuwa mkazi wa kata ya Nainokanoka, amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapa elimu na kuelewa umuhimu wa kupisha eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na hatimaye kuamua kuhama kwa hiari na kuelekea maeneo mengine ambayo Serikali ya awamu ya sita imewapangia.


"Sisi tumeamua kuhama kwa hiari yetu wenyewe bila kulazimishwa ili kupisha eneo la Hifadhi, zipuuzeni habari za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya vyombo  vya habari, tunalazimishwa kuhama, tumeelilishwa na kuelewa umuhimu wa hifadhi yetu, ambayo ni urithi wa Dunia " 


Naye Theresia Sabore Moko, amempongeza na kumshukuru Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuziandalia familia zao makazi mapya nje ya eneo Hifadhi, eneo ambalo mara kwa mara familia zao, zilijeruhiwa na wanyama, na wengine walipoteza maisha kwa kushambuliwa na wanyama.


"Mimi na familia yangu, tumeamua kujiandikisha kwa hiari, kuhamia Msomera, eneo ambalo Serikali imetupa bure bila kutoa gharama yoyote,  tumeona ni eneo salama kwa maisha yetu na familia, zaidi tumeamua kuanza maisha mapya na kuanza kufanya shughuli za uzalishaji mali, shughuli ambazo tukiwa ndani ya Hifadhi hatukuruhusiwa kuzifanya kama vile kilimo" Amebainisha Theresia


Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, Richard Kiiza, amefafanua kuwa, kundi hilo limefanya kufikia jumla ya Kaya 264, watu 1,853 na mifugo 6,934 kwa awamu hiyo ya pili, na kuongeza kuwa taratibu zote za malipo ya stahiki za kaya hizo yameshafanyika ikiwa ni pamoja na maandalizi ya mapokezi katika maeneo yote wanayokwenda kuishi.




Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.