Na Elinipa Lupembe.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha, kuboresha ramani iliyoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vinavyozunguka Stendi mpya ya Daladala, Jiji la Arusha, inayotarajiwa kujengwa, kata ya Themi halmashauri ya Jiji la Arusha.
Mhe. Mongella, amemuagiza Mkurugenzi na Mhandisi wa Jiji hilo kuboresha ramani
iliyowasilishwa na kuandaa mchoro mwingine ambao msingi wake utajengwa ghorofa ambalo, ndani yake kuwe na sakafu zaidi ya moja itakayojengwa vibanda kwa ajili ya wafanyabiashara, ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara na wateja wao.
Amesisitiza kuja na mpango wa muda mrefu ambao, unaendana na matumizi bora ya ufinyu wa ardhi Arusha na kuongeza kuwa mpango ambao utadumu kwa vizazi vijavyo, unaoendana na ongezeko la idadi ya watu na sio mipango ya muda mfupi, mbao husababisha usumbufu kwa watumiaji.
Aidha, amewagiza kuhakikisha baada ya kukamilisha ujenzi wa vibanda hivyo, kugawa viwabanda kwa kutangaza tenda, kupitia mfumo wa TAUSI ili wafanyabiashara waweze kupata kwa haki na kwa usawa sambamba na kuondoa migogoro baina ya Jiji na wafanyabiashara.
Licha ya kuwataka kujenga stendi ya kisasa, ambayo ina miundombinu yote ya kutolea huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuandaa mikataba thabiti itakayoondoa migogoro ambayo inalisumbua jiji la Arusha kwa miaka mingi sasa.
"Jengeni vibanda vyenye viwango vya ubora unaoendana na wafanya biashara wa kisasa, ili viweze kudumu vizazi vijavyo, jambo ambalo hili litaleta kwa wananchi na kuacha sifa kwa uongozi hata mtaka na sio kuacha migogoro". Amesema
Akiwasilisha taarifa mradi huo, Mhandisi Jacob Mwakyambiki, amesema kuwa, mradi huo, utagharimu shilingi milioni 300 na unatarajia kukamilika mapema meezi Aprili , 2024,
Lengo la mradi huo ni kupunguza msongamano katikati ya mji na kuondoa adha ya magari kushusha na kupakia maeneo yasio rasmi hususani pembezoni mwa barabara ndani ya Jiji la Arusha.
Awali, Mhe. Mongella ametoa maagizo hayo, wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo la ujenzi wa stendi mpya ya Daladala, leo 21 Desemba, 2023.
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.