Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ameuagiza uongozi wa TANESCO mkoa na wialaya ya Karatu, kushirikiana na TEMESA, ili kufanikisha zoezi la kufunga umeme mkubwa 'phase 3' kwenye hospitali ya wilaya ya Karatu, ili mashine zilizofungwa hospitalini hapo hususani mashine ya mionzi 'X- ray', ianze kufanya kazi ya kutoa huduma, kwa wananchi kama yalivyo malengo ya Serikali.
Amesema kuwa, Serikali imeshaleta vifaa tiba kwenye hospitali hiyo, lakini bado vinashindwa kutoa huduma kwa wananchi, kwa kukosekana na umeme wenye uwezo wa kuendesha mashine hiyo, jambo ambalo halivumiliki, na kusisitiza kuwa, hali hiyo ni kutokuwatendea haki wananchi wa Karatu.
"Mashine ipo hapa, nini kinashindikana kufunguza umeme unaohitajika? TANESCO shirikianeni na TEMESA, kuhakikisha vifaa vinavyohitajika vinafungwa, ninawapa wiki mbili, nitarudi hapa, umeme uwe umefungwa na X - ray iwe imeanza kuhudumia wananchi, tuwahurumie wananchi hawa" Asemema
Aidha amewataka watumishi wa Umma, kila mmoja kuwajibika katika nafasi yake, na kusisitiza kuwa Serikali imewaajiri na kuwapa dhamana kupitia taaluma zao, kulitumikia Taifa, wakiwa na jukumu kubwa la kuwahudumia wananchi, wasipo wajibika, wanaoteseka ni wananchi.
"Mtumishi anaposhindwa kuwajibika kwenye nafasi yake, wanaoteseka ni wananchi, vifaa hivi viko hapa muda mrefu, kuna mtu au watu wameshindwa kutimiza wajibu wao, kama kila mtumishi wa Umma akitimiza wajibu wake, tutafikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi" Ameweka wazi Mhe. Mongella
Amesisitiza kuwa, Serikali chini ya Mhe Rais Dkt. Samia, inapamaba sana kuhakikisha miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi inawekwa karibu na wananchi, watumishi fanyeni kazi, timizeni majukumu yenu ili kumuunga mkoa Rais na Serikali ya awamu ya sita yenye malengo na nia njema ya kuwahudumia watanzania na wanaKaratu.
"Ninarudia tena na tena kusema, wananchi wanahitaji suluhisho za changamoto zao na sio michakato ya kutatua changamoto, wananchi hawaielewi michakato ya manunuzi, hayo ni mambo yenu, wanachohitaji ni huduma, wajibikeni ili kupata suluhisho la changamoto za watanzania" Amesisitiza Mhe. Mongella.
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.