Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vitano vya Madarasa shule ya Msingi Qaru kata ya Endabashi halmashauri ya Karatu, Mradi uliotekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Kuboresha Upatikanaji wa Fursa sawa katika Ujifunzaji Bora kwa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) kwa gharama ya shilingi milioni 131.3
Kiasi hicho cha fedha kimejumuisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, samani za madarasa pamoja na matundu ya vyoo vya wasichana na wavulana.
Hata hivyo Mhe. Mongella ameushauri uongozi wa halmashauri kujipanga kuanza kufanya ukarabati wa mamajen yaliyoanza kuhakaa kutokana na kujengwa miaka mingi iliyopita, amewataka kufanya ukarabati huo kwa awamu kwa kutumia fedha za uendeshaji shule pamoja na mapato ya ndani.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Qaru, Mwl. Asumpta Ditto, amesema kuwa ujenzi wa madarasa hayo umeondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani kwa kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 975 na kuongeza kuwa kwa sasa wanafunzi wanafurahia uwepo wa madarasa mapya kwa kuwa madarasa yaliyokuwepo ni machakavu kutokana na kujengwa miaka ya 1970, kwa sasa shule imeanza kuwa na mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia.
"Kwa sasa wanafunzi wanafurahia shule, madarasa mapya yamepunguza msongamano wa wanafunzi, tunaamini mazingira haya rafiki yataongeza ari ya kusoma na kupandisha taaluma shuleni" Amebaimisha Mwl. AsuAsump
Hata hivyo Mwl. Asumpta amesema kuwa majengo ya shule hiyo yalijengwa miaka ya 70 na sasa yameanza kuchakaa na kuiomba serikali kuafanya ukarabati mkubwa wa majengo hayo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.